TARURA

Tangazo la Zabuni ya Utozaji wa Ada za Maegesho ya Vyombo vya Usafiri Kwenye Hifadhi za Barabara za Halmshauri ya Kibaha Mji, Halmashauri ya Bagamoyo, Halmashauri ya Chalinze, Halmashauri ya Mkuranga, na Halmashauri ya Kibaha Mkoa wa Pwani

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

WAKALA WA BARABARA ZA VIJIJINI NA MIJINI (TARURA)

TANGAZO LA ZABUNI

ZABUNI NA. AE/2019-2020/CR/NC/11

YA

WAKALA WA UTOZAJI WA ADA ZA MAEGESHO YA VYOMBO VYA USAFIRI KWENYE HIFADHI ZA BARABARA ZA HALMASHAURI YA KIBAHA MJI, HALMASHAURI YA BAGAMOYO, HALMASHAURI YA CHALINZE,HALMASHAURI YA MKURANGA NA HALMASHAURI YA KIBAHA MKOA WA PWANI

Tarehe: 24/05/2019

1. Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) Mkoa wa Pwani unakusudia kutumia huduma za Wakala kutoza ada za maegesho ya vyombo vya usafiri katika maeneo ya hifadhi za barabara zote zilizo chini ya usimamizi wake katika Halmashauri ya Kibaha Mji, Halmashauri ya Bagamoyo, Halmashauri ya Chalinze, Halmashauri ya Mkuranga, na Halmashauri ya Kibaha.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) unapenda
kuwakaribisha waombaji wenye sifa kutuma maombi yao kwa ajili ya zabuni ya Wakala wa Kutoza Ada za Maegesho ya Vyombo vya Usafiri Kwenye Hifadhi za Barabara Katika Halmashauri ya Kibaha Mji, Halmashauri ya Bagamoyo, Halmashauri ya Chalinze, Halmashauri ya Mkuranga na Halmashauri ya Kibaha, Zabuni Namba AE/2019-2020/CR/NC/11

SIFA ZA MUOMBAJI: Muombaji atatakiwa kuwa na sifa zifuatazo
i. Awe Mtanzania
ii. Muombaji awe ni Kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria za Tanzania na ambayo haijawahi kuzuiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kujihusisha na shughuli za Ununuzi wa Umma.
iii. Muombaji awe na mtaji usiopungua Shilingi Milioni Mia Moja
(100,000,000.00) ambao umeainishwa kwenye Memoranda ya Kampuni
(Memorandum and Articles of Association) au ushahidi kuwa kampuni
iliongeza mtaji wake.
iv. Muombaji awe na ofisi ya kudumu anapofanyia kazi zake.
v. Muombaji awe na leseni hai ya biashara ya uwakala wa utozaji wa ada ya maegesho.
vi. Muombaji awe na uzoefu usiopungua miaka miwili kuanzia mwaka 2014 kwenye kazi ya uwakala wa utozaji wa ada ya maegesho ya Vyombo vya Usafiri kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa hususani Majiji,
Manispaa au Taasisi za Serikali.
vii. Muombaji awe na cheti cha Utambulisho wa Mlipa kodi (TIN)
viii. Muombaji awe amesajiliwa kulipa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
ix. Muombaji awe na hati halali ya kuthibitisha ulipaji wa kodi (Tax Clearance)
x. Muombaji awe na taarifa za kifedha zilizokaguliwa (Audited Financial
Statement) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2016 hadi 2018.
xi. Muombaji awe na taarifa za kifedha ya benki (Bank Statement) ya kipindi cha kuanzia tarehe 1 Januari, 2018 mpaka tarehe 30 Aprili, 2019 yenye mauzo (turnover) yasiyopungua Shilingi 100,000,000.00 Taarifa hiyo
iwe na “Certificate of Balance” kutoka katika Benki husika.
xii. Muombaji awe na cheti cha OSHA kinachoonyesha kukidhi matakwa ya
Sheria Na. 5 ya Mwaka 2003
xiii. Muombaji awe amesajiliwa kwenye Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi (WCF) kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Sura ya 263 pitio la Mwaka 2015.
xiv. Muombaji awe na sifa njema ya kufanya kazi ya Uwakala wa kukusanya ada za maegesho ya vyombo vya usafiri kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa hususani Manispaa na Majiji, Manispaa au Taasisi za Serikali
xv. Asiyewahi kuwa na mashauri katika chombo chochote cha Kisheria
kuhusiana na mkataba wa aina yoyote na Taasisi yoyote ya Serikali.

4. Zabuni zitashughulikiwa kwa utaratibu wa ushindani wa kitaifa [National Competitive Bidding] ulioainishwa kwenye Kanuni za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2013, zikisomwa pamoja na marekebisho yake ya Mwaka 2016 na ziko wazi kwa waombaji wote wa hapa nchini.

5. Waombaji wote wenye nia na uwezo wanaweza kupata taarifa kamili kupitia makabrasha ya zabuni katika ofisi ya Katibu wa Bodi Kasimu ya Zabuni TARURA Mkoa wa Pwani, kupitia anuani iliyotajwa hapo juu kila siku kuanzia saa mbili kamili (02.00) asubuhi hadi saa tisa (09:00) kamili alasiri, siku za Jumatatu hadi Ijumaa [isipokuwa siku za sikukuu zinazotambulika kitaifa].

6. Muombaji atatakiwa kujaza kwa usahihi na kuwasilisha Fomu ya dhamana ya zabuni (Bid Securing Declaration) kwa muundo ukatika muundo wa Bid Securing Declaration inayopatikana kwenye kabrasha la zabuni.

7. Nyaraka za Zabuni zitapatikana baada ya kulipa ada stahiki ya zabuni ya Shillingi Laki Moja tu (TZS 100,000.00) Kupitia akaunti namba 53010001080
iliyopoiliyopo katika Benki ya NMB, TARURA Collection Account Muombaji atatakiwa kuwasilisha nakala halisi ya hati ya malipo ya Benki ikiambatana na barua ya maombi ya Zabuni husika. Malipo yaliyotolewa kama ada ya maombi ya zabuni hayatarejeshwa.

8. Zabuni zote ziwe na nakala halisi (original) moja (1) na nakala (copies) tatu (3) zinazofanana zifungwe ndani ya bahasha iliyofungwa kwa lakiri na juu ya bahasha ziandikwe maelezo ya Zabuni na kisha iandikwe na kuwasilishwa kwa anuani ifuatayo: Katibu wa Bodi Kasimu ya Zabuni TARURA ya Mkoa wa PWANI, S. L. P. 30458, Pwani katika jengo la “Chama Cha Walimu Tanzania” – Ghorofa ya Kwanza Chumba No. 03

9. Siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya zabuni ni tarehe 07/06/2019 kabla ya saa 05:30 asubuhi. Zabuni zitafunguliwa hadharani mara tu baada ya muda wa mwisho wa kuwasilisha zabuni, waombaji wote au wawakilishi wao wanaalikwa kuhudhuria ufunguzi wa zabuni hizo utakao fanyika siku hiyo katika ofisi ya Mratibu wa TARURA Mkoa wa Pwani.

10. Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) hautalazimika kukubali/ kutokukubali kutoa zabuni kwa mwombaji yeyote kutokana na kigezo cha malipo makubwa/malipo kidogo ya zabuni.

11. Zabuni zitakazochelewa kuwasilishwa, zabuni za kielektroniki, na zabuni zisizofunguliwa katika tukio la ufunguaji zabuni, kwa hali yoyote ile hazitakubaliwa
kwa tathmini.

……………………………….
MRATIBU WA MKOA – PWANI,
WAKALA WA BARABARA ZA VIJIJINI NA MIJINI
TANZANIA (TARURA)

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related