SAUTI

Tangazo la Zabuni ya huduma ya chakula SAUT-MWANZA

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Chuo Kikuu cha Mt. Agustino (SAUT-MWANZA),

TANGAZO LA ZABUNI ya huduma ya chakula

Zabuni No. SAUT/10/2019/2020

Chuo Kikuu cha Mt. Agustino (SAUT-MWANZA), kinatangaza zabuni ifuatayo: Zabuni ya Huduma ya Chakula

Zabuni inatanza mwaka unaoanzia 1st September, 2019 -31th August 2020.

Vigezo vya jumla:
(i) Kuwa tayari kutoa huduma katika maeneo ya chuo atakayopangiwa na uongozi wa chuo
(ii) Awe na leseni ya biashara inayohusiana na shughuli atakayoifanya.
(iii) Awe na vyeti vya uthibitisho kutoka mamlaka zinazohusika na shughuli yake (TFDA, TRA, JESHI LA POLISI, nk)
(iv) Awe tayari kuthibitisha uwezo wa kifedha alionao wa kuendesha shughuli hizo kwa ufanisi.

Vigezo vya ubobezi:
•HUDUMA YA CHAKULA
(i) Awe na uzoefu wa kutoa huduma ya chakula usiopungua miaka miwili.
(ii) Awe tayari kuthibitisha uwezo wa kitaaluma wa kutoa huduma ya chakula
(i) Awe na uzoefu wa kutoa huduma hiyo usiopungua miaka mitatu
(ii) Awe tayari kutoa huduma Chuoni Nyegezi, Malimbe, Nyumba zawafanyakazi na mashambani.
(iii) Awe na walinzi waliofuzu katika fani ya ulinzi, waliopata mafunzo stahiki
(Paramilitary)
(iv) Awe na walinzi waliohakikiwa kuwa hawajahusika na makosa ya jinai
(Vetted by Police to be crime free)
(v) Kwa wale watakaokuwa katika zabuni ya sehemu za kuendesha biashara na ulinzi wanakaribishwa kuja kuyatembelea maeneo yatakayohusika
katika shughuli zao siku ya Jumatatu Augosti 5,2019 saa tatu asubuhi.

UTARATIBU WA KUSHIRIKI
A. Kwa Wazabuni watakaotaka kushiriki kwenye mchakato huu wanapaswa
kununua nyaraka za Uzabuni (Tender Document) kwa gharama ya Shs.
150,000/=. Walipe fedha hizo kwa jina Mt. Augustina (S.A.U.T)Account
No. 015101001461.bank NBC

B. Utaratibu wa kupata nyaraka za Uzabuni (Tender Documents)
Mara baada ya kulipia bank, Mzabuni afike ofisi ya manunuzi (Purchasing
and Supplies unit) MALIMBE Campus jengo la Utawala kuchukua fomu
akionyesha stakabadhi ya malipo ya bank.
(i) Anatakiwa kurudisha nyaraka hiyo ikiwa imefungwa kwenye
bahasha iliyoandikwa kumbukumbu ya ZABUNI No. SAUT/10/2019/2020 na kutumbukiza kwenye Sanduku la Zabuni litakalokuwa kwenye ofisi ya kumbukumbu(Procurement Management Unit-PMU) kabla ya tarehe
12,Augosti,2019, saa kumi jioni (4:00pm)

(ii) Maombi yatakayoletwa baada ya wakati na siku iliyotajwa
Hayatapokelewa.
(iii) Maombi yatumwe kupitia anwani hii;

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Utawala na Fedha CDVCAF)
Chuo Kikuu cha Mt. Augustino cha Tanzania
S.L.P. 307,
Mwanza-Tanzania
Tel: +2557362009943
Email: [email protected]
Website: www.saut.ac.tz

(iv) Maombi ya Zabuni (Bids) yatafunguliwa tarehe 15 Augosti 2019 kwenye
chumba cha LAVOIRE CENTRE-SAUT, saa tisa mchana. Mbele ya
Wazabuni au Wawakilishi wao.
(v) Chuo kitamtaarifu Mzabuni aliyeshinda kwa maandishi.
(vi) Chuo hakibanwi kutoa zabuni kwa mshindani aliyetoa bei ya chini.
(vii) Chuo hakitawajibika kutoa sababu kwa wale watakaoshindwa kupata
Zabuni

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related