UDSM LOGO

TANGAZO LA MNADA WA HADHARA WA MALI NA VIFAA CHAKAVU

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

TANGAZO LA MNADA WA HADHARA WA MALI NA VIFAA CHAKAVU

Wananchi wote mnatangaziwa kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampasi ya Mwil. J.K. Nyerere Miimani na Taasisi ya Sayansi za Bahari Zanzibar vitauza kwa njia ya mnada wa hadhara mali na vifaa chakavu kuanzia tarehe 12/10/2022 saa nne kamili (4:00) asubuhi.

Mali zitakazouzwa ni:

1. Magari 6. Vifaa mbalimbali vya ofisi

2. Pikipiki 7. Vifaa vya Maabara

3. Samani za ofisi 8. Magodoro

4. Vifaa vya Tehama 9. Vifaa vingine chakavu

5. Boti chakavu

VIGEZO NA MASHARTI YA MNADA

1. Mali/kifaa kitauzwa kama kilivyo na mahali kilipo kwa mnunuzi wa bei ya juu kuliko wote.

2. Mnunuzi atalazimika kulipa fedha taslimu papo hapo ikiwa ni malipo ya awali ambayo si chini ya asilimia ishirini na tano (25%) ya thamani ya chombo husika (Gari /Pikipiki).

3. Mnunuzi akishindwa kutimiza sharti hili, atapoteza haki zote za ununuzi wa mali husika na malipo ya awali hayatarejeshwa kwake.

4. Mnunuzi atatakiwa kuondosha chombo husika cha usafiri (Gari na Pikipiki) atakachonunua kutoka katika eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampasi ya Mw. J.K. Nyerere Miimani na Taasisi ya Sayansi za Bahari Zanzibar ndani ya siku saba (7) kuanzia siku ya kukamilisha malipo ya mwisho.

5. Kwa vifaa vya samani za ofisi, vifaa vya TEHAMA, vifaa mbalimbali vya ofisi, vifaa vya Maabara, Magodoro na vifaa vingine chakavu n.k., mnunuzi atalazimika kulipa fedha taslimu siku hiyo ya mnada wa hadhara kwa asilimia mia moja (100%) ya thamani yote na kuondosha kifaa/vifaa atakavyonunua siku hiyo ya mnada kabla ya saa kumi na mobili (12) jioni.

6. Vifaa vitakavyouzwa vinaweza kukaguliwa siku mbili (2) kabla ya tarehe ya mnada.

Makamu Mkuu wa Chuo

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

S.L. P. 35091

Dar es Salaam

Namba ya simu: +255-22-2410700 na 2410500-8, Tawi 2001

Nukushi: +255-22-2410078/2410023/2410512

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related