Close

June 25, 2020

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Tarehe 08 Julai,2020 Halmashauri ya Wilaya ya Busega

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Kumb.Na.BDC/C.30/17/60

23 Juni, 2020

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI.

Kutokana na Tangazo la nafasi za kazi lenye Kumb.Na. BDC/C.30/17/58 la tarehe 06 Mei, 2020 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega anatarajia kuendesha Usaili na hatimae kuwapangia vituo vya kazi waombaji watakao faulu usaili.

Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa wazingatie mambo Muhimuyafuatayo;
•Usaili utafanyika tarehe 08 Julai,2020kuanzia saa 2:30 Asubuhi Usaili wa mchujo/Vitendo na tarehe 09Julai, 2020Usaili wa mahojiano (kwa watakaofanikiwa) katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Nyashimo.
•Ukaguzi wa vyeti utaanza saa 1:30 asubuhi kabla ya muda wa mtihani wa mchujo/usaili wa vitendo kuanza.
•Kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. Mfano, Kitambulisho cha mkazi, kupiga kura, kazi, Hati ya kusafiria n.k.
•Kuja na vyetiHALISI (Original Certificates) na HALALIvya kuanzia kidato cha Nne, Sita, Astashahada, Stashahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.
•Kuja na Cheti Halisicha kuzaliwa (ORIGINAL BIRTH CERTIFICATE).
•Testimonials “Provisional Results”, “Statement of Results” Hati ya matokeo ya kidato cha Nne na Sita (FORM IV AND FORM VI) HA VITAKUBALIKA.
•Kila Msailiwa Atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
•Kwa waombaji ambao majina yao hayakuonekana katika Tangazo hili, watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisiste kuomba tena mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.

Orodha ya waombaji walioitwa kwenye usaili ni kama inavyoonekana hapa chini


KUSOMA MAJINA HAYO PAKUA PDF HAPO CHINI