Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Tume ya Utumishi wa Mahakama

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA

TANGAZO KWA UMMA

KUITWA KWENYE USAILI

1.0. Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa
mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Sheria ya
Uendeshaji wa Mahakama Na. 4/2011, Tume ya Utumishi wa
Mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine inalo jukumu
la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama.

2.0. Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia
wafuatao ambao waliomba nafasi za ajira za Hakimu Mkazi
Daraja la II, Wasaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II, Msaidizi
wa Maktaba, Makatibu Mahsusi Daraja la III, Wasaidizi wa
Ofisi, Walinzi na Madereva Daraja la II, wafike kwenye usaili
kwa tarehe zilizoonyeshwa hapo chini. Aidha,

A. Usaili kwa ajili ya Hakimu Mkazi Daraja la II utafanyikia
katika Chuo cha Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (Law
School of Tanzania) kuanzia saa 2:00 Asubuhi kwa kila siku
na tarehe iliyoonyeshwa hapo chini.

B. Usaili kwa ajili ya nafasi za Wasaidizi wa Kumbukumbu
Daraja la II, Makatibu Mahsusi Daraja la III, Msaidizi wa
Maktaba II, Walinzi, Wasaidizi wa Ofisi na Madereva Daraja
la II, utafanyika kwenye kumbi zilizoko ndani ya uwanja
mpya wa Taifa (National Stadium) unaotazamana na Ofisi
ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

KUONA MAJINA HAYO PAKUA HIYO PDF