Chuo Mahakama

Mafunzo ya Udalali Mahakama na Usambazaji wa Nyaraka za Mahakama

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO

TANGAZO KWA UMMA

  1. Chuo cha Uongozi wa mahakama Lushoto kinapenda kuutangazia Umma kwamba kinatarajia kufanya mafunzo yanayowalenga wale wote wenye nia ya kuomba na kufanya kazi ya udalali wa Mahakama na Usambaza wa nyaraka za mahakama , Tangazo la Serikali Namba 363 la 20017 ( The court Brokers and Process Servers ( Appointment, Remuneration and Disciplinary) Rules GN. No 363 of 2017)
  2. Muda na Mahali
    Mafuzo yatafanyika kuanzia tarehe 11 Machi 2020 mpaka tarehe 24 Machi 2020 katika Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa vitendo (Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam
  3. SIFA ZA WAOMBAJI:- Muombaji anapaswa kuwa na siifa zifuatazo
    a) Awe Raia na Mkazi wa Tanzania mwenye umri wa utu uzima
    b) Awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza kingereza na kiswahii kwa ufasaha
    c) Awe ni mtu mwenye tabia njema na muadilifu wa kiwango cha juu ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai/yahusuyo uaminifu na uadilifu
  4. MUOMBAJI ASIWE;
    jaji au Hakimu aliyekazini au mwajiriwa wa nafasi yoyote katika Mahakama ya Tanzania au Wakili wa kujitegemea
  5. ADA YA USHIRIKI:l
    Kwa washiriki wa mafunzo ya udalali wa mahakama ada itakuwa ni shilingi 970,000/= kwa washiriki wa mafunzo ya usambazaji nyaraka za mahakama ada itakuwa shilingi 650,000/=
  6. JINSI YA KUTUMA MAOMBI
    waombaji wanaweza kuingia katika tovuti ya chuo www,ija.ac.tz ili kupata fomu ya maombi na kuijza na kuiwakilisha chuoni kwa njia ya Posta (EMS) au kwa anwani ya barua pepe [email protected] au [email protected] ama kufika chuoni na kuiwakilisha kwenye ofisi ya Mkuu wa Chuo

7 FOMU YA MAOMBI IAMBATANISHWE NA :-
a). Kivuli cha cheti elimu ya kidato cha nne na kuendelea
b) kivuli cha cheti cha kuzaliwa au kitambulisho cha uraia
c) nakala ya risiti ya malipo ya ada ya maombi shilingi 30,000/=Malipo ya maombi yafanyike kupitia control Number 995700002411 mlipwaji ni chuo cha uongozi wa mahakama Lushoto

8. Malipo ya maombi yafanyike kupitia control Number 995700002411 mlipwaji ni chuo cha uongozi wa mahakama Lushoto

9. kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya chuo www.ija.ac.tz au piga simu zifuatazo + 255-27-2660133 au 0784893676 au 0658154242

10 .Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 03/02/2020

IMETOLEWA NA

MKUU WA CHUO,
CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO,
S.L.P 20
LUSHOTO

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Related