WAUGUZI NAFASI 4 (Re -advertised)

Full time Sense International Tanzania in Health Care
  • Dar es Salaam, Tanzania View on Map
  • Post Date: November 6, 2018
  • Apply Before : November 12, 2018
  • Applications 0
  • View(s) 263
Email Job
  • Share:

Job Detail

  • Experience 2 Years
  • Industry Management
  • Qualifications Diploma

Job Description

Sense International ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya shughuli za kuhudumia jamii ya watu wenye
ulemavu wa uziwikutoona (Deafblindness) ili waweze kujifunza,kuishi na kufanikiwa. Aidha, shughuli za
shirika zipo nchini Bangladesh, India, Nepal, Tanzania, Peru, Romania na Uganda. Nchini Tanzania, Sense
International inashirikiana na serikali na asasi mbalimbali katika kuwatambua watu wenye uziwikutoona
kisha kuwawezesha kielimu, kiafya na namna ya kujikimu kimaisha ili waweze kushiriki na kuchangia
maendeleo ya jamii.

Ili kuhakikisha ya kwamba mabadiliko ya utoaji huduma yanakuwa endelevu shirika linawekeza katika
kufanya ushawishi wa mabadiliko ya sera ili ziakisi utoaji wa huduma kulingana na mahitaji ya watu wenye ulemavu, kujenga mazingira wezeshi ya utoaji wa huduma za elimu na afya kwa watu wenye uziwikutoona pamoja na kuwaendeleza na kuwatumia wataalamu wazawa.
Hivi sasa Sense International Tanzania kwa kushirikiana na Manispaa ya Temeke inahitaji wauguzi kwa ajili ya kufanya kazi katika mradi wa kufanya Utambuzi na utoaji wa Afua za Mapema (Early Intervention) kwa watoto wenye uziwikutoona na wenye ulemavu mwingine mchanganyiko kuanzia miaka 0-5. Mradi huu ni wa ufadhili wa Jessey Overseas Aid (JOA) kutoka nchini Uingereza.

WAUGUZI –NAFASI 4
Wilaya: Temeke
Mkoa: Dar es Salaam
Muda wa ajira: Miaka 2 au zaidi kutegemeana na uwepo wa ufadhili.
Mshahara: Mshahara mzuri sambamba na marupurupu.

Majukumu ya kazi:
 Kufanya upimaji wa milango ya fahamu (uoni na usikivu) kwa kutumia vifaa maalumu katika vituo
vya kutolea huduma.
 Kutumia dodoso maalumu kubaini viashiria hatarishi kwa watoto ambao bado hawajapimwa na
kutumia vifaa maalumu pale inapohitajika.
 Kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa mtaalamu wa Tiba Liwaza (Occupational Therapist) ili
kuweza kuandaa mpango madhubuti wa utoaji Afua za Mapema kwa watoto wanaopatikana na
uziwikutoona au ulemavu mwingine Mchanganyiko unaopelekea changamoto za mawasiliano na
kujimudu.
 Kutoa ushauri kuhusu changamoto mbalimbali katika vifaa vinavyotumika kuwasaidia watoto
wenye uziwikutoona.
 Kushirikiana na mtaalamu wa tiba liwazo, wazazi na watoto katika kusadia maendeleo ya watoto
wenye uziwikutoona.
 Kutunza kwa makini vifaa vilivyopo katika kituo cha kutolea huduma.
 Kuagiza kwa wakati vifaa muhimu vya kutumiwa katika kituo cha kutolea huduma.
 Kutumia mifumo iliyopo ya kusimamia na kutoa taarifa kuhusu utoaji huduma za Upimaji na Usaidizi
wa awali.
 Kushiriki katika kuelimisha jamii kuhusu huduma ya upimaji na usaidizi wa awali katika kituo cha
kutolea huduma katika jamii na mahali pengine utakapohitajika.
Tunatafuta muuguzi mwenye uzoefu katika kazi ya uguuzi, kuhudumia watu kwa weledi, kuwasiliana vizuri na kutoa taarifa ya maendeleo kwa wakati na umakini.

Vigezo vya mwombaji:
 Awe na “Diploma” ya uuguzi kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.
 Awe mwanachama wa Baraza la cha Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nursing and Midwifery
Council).
 Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka 2.
 Awe na zoefu wa kusaidia watoto wenye ulemavu hususani watoto wenye Uziwi-kutoona
(Deafblindness).

Kufahamu zaidi kuhusu kazi zetu, tembelea: https://www.senseinternational.org.uk/our-work/tanzania

Kama una vigezo stahiki na ungependa kuomba kazi hii, tuma barua yako ya maombi na wasifu wako kwa

Mkurugezi,
Sense International Tanzania,
P O BOX 72653,
Dar es Salaam.
kupitia infotz@senseint-ea.org.

Unapotuma barua pepe, weka kichwa (SUBJECT) MUUGUZI – TANZANIA. Tafadhali elezea kwenye barua yako ya maombi; sababu za kupendezwa na nafasi hii, ni kwa jinsi gani ujuzi na uzoefu wako unashabihiana na kazi hii, pia elezea mshahara unaopokea sasa pamoja na namba yako ya simu inayopatikana. Mwisho wa kutuma maombi ni saa 11 kamili jioni, tarehe 12 Novemba, 2018. Ni wale tu waliofuzu ndio watapokea majibu.

Sense International inaajiri bila kuzingatia jinsia, dini, rangi, kabila, uraia,hali ya ulemavu au namna yoyote ya ubaguzi.

Other jobs you may like