Wataalamu wa Tiba Liwaza (Nafasi 4)

Full time Sense International Tanzania in Health Care
  • Dar es Salaam, Tanzania View on Map
  • Post Date: November 6, 2018
  • Apply Before : November 12, 2018
  • Applications 0
  • View(s) 307
Email Job
  • Share:

Job Detail

  • Experience 2 Years
  • Industry Management
  • Qualifications Diploma

Job Description

Sense International ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya shughuli za kuhudumia jamii ya watu wenye
ulemavu wa uziwikutoona (Deafblindness) ili waweze kujifunza,kuishi na kufanikiwa. Aidha,shughuli za
shirika zipo nchini Bangladesh, India, Nepal, Tanzania, Peru, Romania na Uganda. Nchini Tanzania, Sense
International inashirikiana na serikali na asasi mbalimbali katika kuwatambua watu wenye uziwikutoona
kisha kuwawezesha kielimu, kiafya na namna ya kujikimu kimaisha ili waweze kushiriki na kuchangia
maendeleo ya jamii.

Ili kuhakikisha ya kwamba mabadiliko ya utoaji huduma yanakuwa endelevu shirika linawekeza katika
kufanya ushawishi wa mabadiliko ya sera ili ziakisi utoaji wa huduma kulingana na mahitaji ya watu wenye ulemavu, kujenga mazingira wezeshi ya utoaji wa huduma za elimu na afya kwa watu wenye uziwikutoona pamoja na kuwaendeleza na kuwatumia wataalamu wazawa. Hivi sasa Sense International Tanzania kwa kushirikiana na Manispaa ya Temeke inahitaji wataalamu wa Tiba liwaza (Occupational Therapist) kwa ajili ya kufanya kazi katika mradi wa kufanya Utambuzi na utoaji wa Afua za Mapema (Early Intervention) kwa watoto wenye uziwikutoona na wenye ulemavu mwingine mchanganyiko kuanzia miaka 0-5. Mradi huu ni wa ufadhili wa Jessey Overseas Aid (JOA) kutoka nchini
Uingereza.

WATAALAMU WA TIBA LIWAZA – NAFASI 4
Wilaya: Temeke
Mkoa: Dar es Salaam
Muda wa ajira: Miaka 2 au zaidi kutegemeana na uwepo wa ufadhili.
Mshahara: Mshahara mzuri sambamba na marupurupu.

Majukumu ya kazi:
 Kuwezesha na kufanya ubaini kama mtoto anafaa kupatiwa Afua za Mapema (Early Intervention
services).
 Kutoa msaada wa kitaalamu wa jinsi ya kuwahudumia watoto wenye uziwikutoona na wale wenye
ulemavu mwingine mchanganyiko katika kukabiliana na changamoto za mawasiliano na kujimudu
kwa kutumia mtaala ulioandaliwa.
 Kutoa ushauri kuhusu changamoto mbalimbali katika utumiaji wa vifaa vinavyotumika kuwasaidia
watoto wenye uziwikutoona.
 Kushirikiana na madaktari, wataalamu wa tiba viungo, maafisa ustawi wa jamii na wauguzi katika
ngazi ya jamii pamoja na familia za watoto wenye uziwikutoona katika mlengo wa kusadia
maendeleo ya watoto wenye uziwikutoona.
 Kusimamia uendeshaji wa kituo cha kufanya utambuzi na utoaji wa Afua za Mapema (Early
Intervention unit).
 Kutunza siri na umakini wa taarifa za watoto wanaohudumiwa kituoni kwa kutumia mifumo ya
analojia na digitali itakayokuwepo kituoni.
 Kuandaa taarifa za wiki na mwezi ili kuzituma kwa mamlaka husika katika kituo cha Afya na Sense
International Tanzania.
 Kushiriki katika kuelimisha jamii kuhusu huduma ya upimaji na usaidizi wa awali katika kituo cha
kutolea huduma, katika jamii na mahali pengine utakapohitajika.
Tunatafuta mtaalamu wa tiba liwaza mwenye uzoefu katika kazi yake, mwenye uwezo wa kuhudumia watu
kwa weledi, kuwasiliana vizuri na kutoa taarifa ya maendeleo kwa umakini.

Vigezo vya mwombaji:
 Awe na “Diploma”ya Tiba Liwaza (Occupational Therapy) kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.
 Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili.
 Uzoefu wa kudumia watoto wenye ulemavu hususani wenye uziwi-kutoona (Deafblindness).

Kufahamu zaidi kuhusu kazi zetu, tembelea: https://www.senseinternational.org.uk/our-work/tanzania

Kama una vigezo stahiki na ungependa kuomba kazi hii, tuma barua yako ya maombi na wasifu wako kwa

Mkurugezi,
Sense International Tanzania,
P O BOX 72653,
Dar es Salaam
kupitia infotz@senseint-ea.org.

Unapotuma barua pepe, weka kichwa (SUBJECT) MTAALAMU TIBA LIWAZA – TANZANIA.

Tafadhali elezea kwenye barua yako ya maombi sababu za kupendezwa na nafasi hii, ni kwa jinsi gani ujuzi na uzoefu wako unashabihiana na kazi hii, pia elezea mshahara unaopokea sasa pamoja na namba yako ya simu inayopatikana. Mwisho wa kutuma maombi ni saa 11 kamili jioni, tarehe 12 Novemba, 2018. Ni wale tu waliofuzu ndio watapokea majibu.

Sense International inaajiri bila kuzingatia jinsia, dini, rangi, kabila, uraia,hali ya ulemavu au namna yoyote ya ubaguzi.

Other jobs you may like