Full time Offered Salary :

Mkurugenzi wa Kituo

Email Job
  • Share this Job :

Job Description

JUMUIYA YA KIKRISTO TANZANIA

REF. NO. CCT/AHR/TNK/19/3

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI

Wapendwa nawasalimu katika jina la bwana Yesu Kristo.
Tunapenda kuwatangazia nafasi ya Kazi ya Mkurugenzi wa Kituo cha mafunzo ya Wanawake Morogogo (CCT – Theofil Kisanji Morogoro Women Training Centre)

Sifa za Mwombaji:

i). Awe Mkristo kutoka Wanachama wa CCT.
ii) . Awe na shahada ya Chuo kikuu kinachotambuliwa katika fani ya Uongozi , Uchumi , Sayansi ya Jamii Elimu au Masomo yanayohusiana na hayo.
iii). Awe na ufahamu, Uzoefu na uwezo wa kuongoza na kusimamia uendeshwaji wa Shirika, Kituo au Programu maalum.
iv). Awe na uwezo wa kusimamia mitaala ya mafunzo yanayoendeshwa na kituo ili yaendane na mahitaji ya soko kwa manufaa ya washiriki na jamii.
v). Awe na uwezo wa kupanga, kutafuta, na kusimamia matumizi ya rasilimal mbalimbali zikiwemo fedha.
vi). Awe na uwezo wa kuandaa taarifa zinazoonyesha mafanikio na changaamoto kulingana na mahitaji ya wafadhili mbalimbali (Result Based Reporting).
vii). Awe na uwezo wa kubuni na kuanzisha mafunzo yanayoendana na hitaji la wakati, soko la ajira na kujiajiri.
viii). Awe na uwezo wa kuandika miradi (Project Proposal) na kuitafutia wahisani ili kuendeleza mafunzo ya kituo.
ix). Awe na uwezo wa kuongea na kaundika lugha ya Kiswahili na Kingereza.
x). Awe na uwezo wa kutumia kompyuta na matandao.
xi). Awe na uzoefu wa kazi wa miaka 5 au zaidi katika nagazi za uongozi.
xii). Awe na umri kati ya miaka 35 na 50.

Waombaji wapitishe barua zao kwa Askofu wa Jimbo dayosisi ya Kanisa mwanachama wa CCT (SIO KWA MAKATIBU AU WACHUNGAJI) na ziambatane na CV zao na ziwe na anwani kamili barua pepe na namba ya simu

Mwisho wa Kupokea maombi ni Tarehe 23 April 2019 waombaji watakao kidhi sifa zote zilizotajwa hapo juu na nyinginezo ndio tu watakaoitwa kweney usali. Ajira inatazamiwa kuanza 1 Julai 2019.

Maombi Yatumwe kwa:

Katibu Mkuu
Jumuiya ya Kikristo Tanzania,
S.L.P 1454,
DODOMA.

Au kwa barua pepe
i). [email protected]
ii)[email protected]

Tunatangulizza shukrani zetu kwa kutusaidia kuwapelekea ujumbe huu wahitaji wa nafasi hiyo.
Tunawatakia baraka za Bwana