JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA
TANGAZO LA MTIHANI WA USAILI
Names Call For Job Interview PCCB (TAKUKURU), January 8th, 2022
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) anapenda kuwatangazia watu wote walioomba nafasi ya ajira ndani
ya Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa kwamba mtihani wa usaili wa maandishi (apptitude test) utafanyika Jijini Dodoma siku ya tarehe 8.1.2022.
Mambo Muhimu ya Kuzingatia
1. Tarehe ya usaili ni tarehe 8.1.2022 siku ya Jumamosi;
2. Kwa waombaji ambao wameomba kazi ya Afisa Uchunguzi mtihani wao
utaanza saa 2:30 asubuhi siku hiyo tarehe 8.1.2022;
3. Kwa waombaji ambao wameomba nafasi ya Uchunguzi Msaidizi mtihani
wao utaanza saa 6:00 mchana siku hiyo ya tarehe 8.1.2022;
4. Waombaji walioitwa kwenye usaili huu wahakikishe wanachukua tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19 muda wote wanaposafiri na wanapokuwa kwenye chumba cha mtihani;
5. Majina ya waombaji wote walioitwa kwenye usaili pamoja na eneo la
kufanyia mtihani yanapatikana kwenye wavuti ya TAKUKURU
www.pccb.go.tz
6. Kila mwombaji ajaze taarifa zake binafsi kwenye fomu ambayo
imeambatishwa na orodha ya majina. Fomu pia inapatikana kwenye wavuti
ya TAKUKURU www.pccb.go.tz
7. Fomu ya taarifa binafsi ijazwe kwa umakini na kwa usahihi. Fomu hiyo ni
sehemu ya mtihani wa apptitude test, kwa hiyo mtu atakayejaza vibaya Fomu
hiyo atakuwa ameipoteza nafasi ya kufaulu kwenye usaili huu;
8. Fomu hiyo iwasilishwe siku ya mtihani tarehe 8.1.2022. Msailiwa ambaye
hatawasilisha Fomu hiyo atahesabika kuwa ni miongoni mwa walioshindwa
kwenye usaili.
9. Watakaofaulu kwenye mtihani wa maandishi ndio watakaoitwa kwenye
usaili wa mahojiano (oral interview)
Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu,
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,
Mtaa wa Jamhuri,
S.L.P 1291,
41101 DODOMA.
Names Call For Job Interview PCCB (TAKUKURU), January 8th, 2022
Majina ya Usaili PCCB-TAKUKURU (Call For Job Interview PCCB).
Tanzania’s first anti-corruption agency dates back to 1974 when Act No.
In July 2007, the Prevention of Corruption Act (PCA) was abolished and
replaced by the current Prevention and Combating of Corruption Act
(PCCA) which renamed the PCB the “Prevention and Combating of Corruption
Bureau” (PCCB).
Call For Job Interview PCCB (TAKUKURU), January 8th, 2022
Director
General of the Institute for the Prevention and Combating of Corruption
(PCCB) would like to announce to all people who have applied for a job
vacancy of the Institute for Prevention and Combating Corruption that
apptitude test will be held in Dodoma on 8.1.2022.
ADVERTISEMENT
For more information get attached PDF file below:-
Download PDF File
Download names in attachment below:-