New Post

Wednesday, November 24, 2021

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) limetoa nafasi za kazi

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


 

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

 

              Ref.No.JA.9/270/01/A/1                                                                      23 Novemba, 2021

 

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifana uwezo wa kujaza nafasi Moja (01) kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.

 

1.0 BARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA (BAKITA)

 

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) liliundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 27 ya mwaka 1967 na kufanyiwa marekebisho madogo mwaka 1983 na 2016 kwa ajili ya kuratibu na kusimamia maendeleo na matumizi ya lugha ya Kiswahili.

 

1.0.1 MCHUNGUZI LUGHA MKUU DARAJA II (Nafasi 1)

                        1.0.1.1      MAJUKUMU YA KAZI

i.           Kusimamia sehemu ya utafiti

ii.          Kushughulikia mambo yahusuyo masomo ya Kiswahili kwa wageni.

iii.         Kutoa mwongozo kwa waandishi na wachapishaji vitabu kuhusu uandishi Bora.

iv.        Kuratibu warsha, semina na mikutano ya kamati ya lugh na fasihi.

v.          Kusimamia kazi ya utoaji ushauri kwa wanafunzi wa sekondari na vyuo     wanapoandika kazimradi.

vi.        ANAWEZA KUTEULIWA KUWA MKUU WA IDARA

     vii.      Kufanya kazi nyingine atakayopangiwa na mkuu wake wa kazi

 

 

1.0.2 SIFA ZA MWOMBAJI

      Shahada ya kwanza na ya Uzamili katika Masomo ya fasihi, Lugha au isimu ya Kiswahili kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na Serikali.

      Uzoefu wa kazi usiopungua miaka nane 

      Awe ameandika makala yoyote au kitabu kinachohusu fasihi au isimu ya lugha ya Kiswahili kama vile tasnifu.

 

1.0.3 Mshahara 

PGSS 10

 

MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i.     Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45. ii.         Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii.           Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iv.           Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

v.            Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.

-      Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

-      Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

-      Computer Certificate

-      Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

vi.           Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

vii.         Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).

viii.        Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

ix.           Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

x.            Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 7, Disemba, 2021.

Muhimu, kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa; KATIBU

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA S.L.P. 2320 DODOMA.

i.        Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/

(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa Recruitment Portal’)

 

ii.      Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Limetolewa na;

 

KATIBU

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA