New Post

Friday, October 29, 2021

Job Vacancy, HEAD MASTER AT Josiah Girls’ High School

 NAFASI YA KAZI: MWALIMU MKUU

Shule ya Josiah Girls’ High School inatangazanafasi ya kazi ya Mwalimu Mkuu.

Kuhusu Shule:Shule ilianzishwa mwaka 2011, Bukoba, Kagera. Ni shule ya bweni na niya wasichana tu. Ina michepuo ya sayansi, sanaa na biashara. Kwa sasa ina wanafunzi zaidi ya mia nne (400), kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Ina wafanyakazi wa taaluma na waendeshaji thelathini na saba (37)

Wajibu/ Majukumu ya Mwalimu MkuuMwalimu mkuu atatakiwa kuwa:

1. Kiongozi Mkuu wa Mambo yote ya Taaluma, Utawala, Taaluma na

Ufundi:

2. Mtunza Hazina: Bajeti, Matumizi na Mapato;

3. Kusimamia nidhamu kwa ujumla: Wanafunzi, Walimu, na waendeshaji

4. Kuhakiki shughuli zote za Ulipaji Kodi na Taarifa ya kila Mwaka ya

Mapato na Matumizi;

5. Kufundisha masomo yake kwa kuzingatia ratiba, muda na nafasi;

Wasifu wa Mwombaji:

Muombaji anatakiwa awe Mwanamke na awe na:

  •  Shahada ya awali katika Nyanja yoyote
  •  Umri usiozidi miaka arobaini na tano (45)
  •  Uzoefu wa kutosha katika kuendesha shule ya sekondari
  •  Uwezo wa kujituma na kusimamia uendeshaji wa shule

Namna ya Kutuma Maombi

Kila muombaji wa kazi hii awasilishe barua ikiwa imeambatana na:

  •  Wasifu binafsi (CV) ukionesha majina matatu ya wadhamini na mawasiliano yao
  •  Cheti cha kuzaliwa na vivuli vya vyeti vya Elimu

Maombi yote yatumwe kupitia barua pepe: anneyyamungue@gmail.

com. Mwisho kupokea maombi ni Tarehe 15 Novemba, 2021.