New Post

Tuesday, February 16, 2021

OPERETA WA KOMPYUTA MSAIDIZI – TGS.B (Nafasi 1)- Tume ya Utumishi wa MahakamaSifa:-


Waombaji waliomaliza kidato cha nne au sita wenye Astashahada ya mwaka mmoja ya masomo ya awali ya Kompyuta yanayojumuisha Uendeshaji wa Kompyuta wa Msingi (Basic Computer Operations), Programu Endeshi (Operating Systems) na Program Tumizi (Applications Program) au Fundi Sanifu wa Kompyuta kutoka kwenye Taasisi/Chuo kinachotambuliwa na Serikali.


Kazi za kufanya:-


(a) Kuchambua taarifa zilizopo kwenye nakala ngumu ili ziwe tayari kuingizwa kwenye mifumo ya TEHAMA


(b) Kuingiza taarifa kwenye mifumo ya TEHAMA


(c) Kuanzisha mchakato wa program za mifumo ya TEHAMA,


(d) Kuangalia mwenendo wa utendaji kazi wa mfumo wa TEHAMA,


(e) Kutoa nakala ngumu na laini ya ripoti mbalimbali kutoka katika mifumo ya TEHAMA,


(f) Kuhifadhi taarifa zinazoingizwa kwenye program tumizi,


(g) Kutunza kumbukumbu za kazi zilizofanyika katika program tumizi, na


(h) Kusahihisha makosa yanayotokea katika taarifa zilizofanyiwa mchakato katika program za mifumo ya TEHAMA.Mwisho wa kupokea barua za maombi hayo ni tarehe 1/3/2021 saa 9:30 Alasiri.


Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji zikionyesha anwani sahihi pamoja na namba ya simu na kuambatisha:-


- Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.


- Wasifu wa mwombaji (CV).


- Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.


- Picha mbili za rangi (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni ambazo zimeandikwa majina nyuma yake .


NB. Nakala za vyeti vya taaluma na vya kidato cha nne/sita vithibitishwe na Hakimu/Wakili anayetambuliwa na Serikali (True copies of the originals).


Aidha, inasisitizwa kwamba:-Waombaji wawe na umri kati ya miaka 18 na 44.


Maombi yote yapitishwe kwa Katibu Tawala wa wilaya anayoishi mwombaji.


Waombaji walio katika Utumishi wa Umma wapitishe maombi yao kwa waajiri wao wa sasa.Waombaji walioacha kazi katika Utumishi wa Umma waeleze kwamba waliacha kazi Serikalini na sababu ya kufanya hivyo.


Waombaji watakao shinda usaili na kuajiriwa watakuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wawe tayari kufanya kazi katika mikoa na Wilaya mbalimbali za Tanzania bara.


Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao vithibitishwe na TCU/NACTE.


Waombaji waandike majina yao yote matatu kwa kirefu.


Waombaji waandike nafasi ya kazi wanayoomba nyuma ya bahasha watakazotumia maombi yao.


Waombaji wasiwe walioachishwa/kufukuzwa kazi kwenye Utumishi wa Umma.


     Waombaji ambao wataficha ama kutoonyesha kwenye viambatisho vyao sifa yoyote ya kielimu waliyonayo na ikabainika wakati wa mchakato wa kuwaajiri mchakato huo utasitishwa na hata kama watakuwa tayari wameajiriwa, ajira zao zitasitishwa mara moja.


    Mwombaji asiandike barua zaidi ya moja kwa ajili ya kuomba nafasi moja.


   Waombaji wote wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia mojawapo ya masharti yaliyotajwa hapo juu, maombi yao hayatashughulikiwa.


Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P. 8391,


DAR ES SALAAM.

Imetolewa na ;-

Katibu,

Tume ya Utumishi wa Mahakama,

S.L.P 8391,

DAR ES SALAAM,