New Post

Tuesday, February 16, 2021

DEREVA DARAJA LA II (Driver II) - TGS B – (Nafasi 10)-Tume ya utumishi wa Mahakama
Sifa:-


(a) Waombaji wawe na  cheti cha kidato cha nne (Form IV) na Leseni ya


Daraja la E au C1 ya uendeshaji Magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.


(b) Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.


(c) Waombaji wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza. 

Kazi za kufanya:-


(a) Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,


(b) Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi,


(c) Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,


(d) Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,


(e) Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari,


(f) Kufanya usafi wa gari, na


(g) Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.


Mwisho wa kupokea barua za maombi hayo ni tarehe 1/3/2021 saa 9:30 Alasiri.


Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji zikionyesha anwani sahihi pamoja na namba ya simu na kuambatisha:-


- Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.


- Wasifu wa mwombaji (CV).


- Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.


- Picha mbili za rangi (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni ambazo zimeandikwa majina nyuma yake .


NB. Nakala za vyeti vya taaluma na vya kidato cha nne/sita vithibitishwe na Hakimu/Wakili anayetambuliwa na Serikali (True copies of the originals).


Aidha, inasisitizwa kwamba:-Waombaji wawe na umri kati ya miaka 18 na 44.


Maombi yote yapitishwe kwa Katibu Tawala wa wilaya anayoishi mwombaji.


Waombaji walio katika Utumishi wa Umma wapitishe maombi yao kwa waajiri wao wa sasa.Waombaji walioacha kazi katika Utumishi wa Umma waeleze kwamba waliacha kazi Serikalini na sababu ya kufanya hivyo.


Waombaji watakao shinda usaili na kuajiriwa watakuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wawe tayari kufanya kazi katika mikoa na Wilaya mbalimbali za Tanzania bara.


Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao vithibitishwe na TCU/NACTE.


Waombaji waandike majina yao yote matatu kwa kirefu.


Waombaji waandike nafasi ya kazi wanayoomba nyuma ya bahasha watakazotumia maombi yao.


Waombaji wasiwe walioachishwa/kufukuzwa kazi kwenye Utumishi wa Umma.


     Waombaji ambao wataficha ama kutoonyesha kwenye viambatisho vyao sifa yoyote ya kielimu waliyonayo na ikabainika wakati wa mchakato wa kuwaajiri mchakato huo utasitishwa na hata kama watakuwa tayari wameajiriwa, ajira zao zitasitishwa mara moja.


    Mwombaji asiandike barua zaidi ya moja kwa ajili ya kuomba nafasi moja.


   Waombaji wote wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia mojawapo ya masharti yaliyotajwa hapo juu, maombi yao hayatashughulikiwa.


Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P. 8391, DAR ES SALAAM.Imetolewa na ;-

Katibu,

Tume ya Utumishi wa Mahakama,

S.L.P 8391,

DAR ES SALAAM,