New Post

Wednesday, February 10, 2021

AFISA USTAWI WA JAMII DARAJA II at Halmashauri ya Wilaya ya Nzega

 POST AFISA USTAWI WA JAMII DARAJA II – 1 POST
POST CATEGORY(S) SOCIOLOGY, POLITICAL SCIENCE, COMMUNITY AND SOCIAL DEVELOPMENT
EMPLOYER Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (NZEGA DC)
APPLICATION TIMELINE: 2021-02-09 2021-02-23
JOB SUMMARY NA
DUTIES AND RESPONSIBILITIES

i.Kuendesha Usaili wa wahudumiwa (watu wenye ulemavu, wazee, familia zenye matatizo, watoto na vijana wenye matatizo mbalimbali);

ii.Kufanya ukaguzi wa mazingira wanayoishi wahudumiwa ili kupata taarifa zao kamili;

iii.Kuandaa taarifa za usaili na ukaguzi wa mazingira ya wahudumiwa;

iv.Kupokea na kukusanya taarifa za Ustawi wa Jamii kutoka kwa wadau na vituo mbalimbali vya Ustawi wa Jamii;

v.Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu huduma za watu wenye ulemavu, wazee, malezi ya watoto na familia zenye matatizo;

vi.Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya uandikishaji vituo vya kulelea watoto wadogo mchana, malezi ya kambo (foster care) na vituo vya walezi wa watoto wadogo mchana;

vii.Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya msaada wa Rais kutoka kwa akina mama, waliojifungua watoto watatu au zaidi kwa mara moja;

viii.Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya watoto yatima au wanaohitaji misaada mbalimbali;

ix.Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali toka kwenye familia za watu wenye dhiki;

x.Kuhoji na kuandaa taarifa za washitakiwa;

xi.Kusimamia wahudumiwa katika makazi, vyuo vya mafunzo ya Ufundi Stadi vya watu wenye ulemavu, Mahabusu za watoto na shule za maadilisho; na

xii.Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake

QUALIFICATION AND EXPERIENCE
Kuajiriwa wenye Shahada au Stashahada ya juu ya Sanaa katika fani ya ‘Social Works’ au ‘Sociology’ kutoka Chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na Serikali

REMUNERATION TGS D

The deadline for submitting the application is 23 February, 2021

TO APPLY CLICK HERE