New Post

Tuesday, February 16, 2021

AFISA UGAVI DARAJA LA II (SUPPLIES OFFICER II) –TGS.D (Nafasi 5)- Tume ya Utumishi wa MahakamaSifa:-


Waombaji wawe na Shahada/Stashada ya juu ya Ununuzi/Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali AU wenye “Professional level III” inayotolewa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini (Procurement and Supplies Professionals and Technicians Board – (PSPTB) au sifa nyingine inayolingana na hiyo inayotambuliwa na PSPTB, ambaye amesajiliwa na PSPTB kama “Graduate Procurement and Supplies Professional”.


Kazi za kufanya:-


(a) Kutayarisha makisio ya vifaa vinavyohitajika (Schedule of Requirements).


(b) Kuandaa utaratibu wa upokeaji wa vifaa


(c) Kukusanya na kutunza takwimu za upokeaji, utunzaji na usambazaji wa vifaa.


(d) Kusimamia upokeaji, utunzaji na usambazaji wa vifaa (Physical Distribution).


(e) Kubuni mfumo wa uwekaji na utunzaji wa vifaa ghalani (Location Index Design).


(f) Kuandaa taarifa mbalimbali za vifaa.


(g) Kuhesabu na kutoa taarifa ya thamani ya vifaa vilivyomo ghalani kwa kufuata taratibu zilizopo.


(h) Kuandaa hati za kupokelea vifaa.


(i) Kutoa vifaa kwa watumiaji (Distribution goods to User department and other users).


(j) Kufanya kazi nyingine za fani yake atakzopangiwa na mkuu wake wa kazi.Mwisho wa kupokea barua za maombi hayo ni tarehe 1/3/2021 saa 9:30 Alasiri.


Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji zikionyesha anwani sahihi pamoja na namba ya simu na kuambatisha:-


- Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.


- Wasifu wa mwombaji (CV).


- Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.


- Picha mbili za rangi (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni ambazo zimeandikwa majina nyuma yake .


NB. Nakala za vyeti vya taaluma na vya kidato cha nne/sita vithibitishwe na Hakimu/Wakili anayetambuliwa na Serikali (True copies of the originals).


Aidha, inasisitizwa kwamba:-Waombaji wawe na umri kati ya miaka 18 na 44.


Maombi yote yapitishwe kwa Katibu Tawala wa wilaya anayoishi mwombaji.


Waombaji walio katika Utumishi wa Umma wapitishe maombi yao kwa waajiri wao wa sasa.Waombaji walioacha kazi katika Utumishi wa Umma waeleze kwamba waliacha kazi Serikalini na sababu ya kufanya hivyo.


Waombaji watakao shinda usaili na kuajiriwa watakuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wawe tayari kufanya kazi katika mikoa na Wilaya mbalimbali za Tanzania bara.


Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao vithibitishwe na TCU/NACTE.


Waombaji waandike majina yao yote matatu kwa kirefu.


Waombaji waandike nafasi ya kazi wanayoomba nyuma ya bahasha watakazotumia maombi yao.


Waombaji wasiwe walioachishwa/kufukuzwa kazi kwenye Utumishi wa Umma.


     Waombaji ambao wataficha ama kutoonyesha kwenye viambatisho vyao sifa yoyote ya kielimu waliyonayo na ikabainika wakati wa mchakato wa kuwaajiri mchakato huo utasitishwa na hata kama watakuwa tayari wameajiriwa, ajira zao zitasitishwa mara moja.


    Mwombaji asiandike barua zaidi ya moja kwa ajili ya kuomba nafasi moja.


   Waombaji wote wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia mojawapo ya masharti yaliyotajwa hapo juu, maombi yao hayatashughulikiwa.


Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P. 8391, DAR ES SALAAM.Imetolewa na ;-

Katibu,

Tume ya Utumishi wa Mahakama,

S.L.P 8391,

DAR ES SALAAM,