New Post

Tuesday, February 16, 2021

AFISA TEHAMA DARAJA LA II - TGS.E – (Nafasi 10)- Tume ya Utumishi wa Mahakama


Waombaji wawe na sifa kama ilivyoorodheshwa hapa chini kutegemea

Fani/Taaluma yake kama ifuatavyo:3.1 Fani ya Utengenezaji Program za TEHAMA (Programming):- (Nafasi 4)


3.1.1 Sifa:-


Waombaji wawe na Stashahada ya Juu au Shahada ya Kompyuta katika moja ya fani zifuatazo; Sayansi ya Kompyuta, Teknolojia ya Habari, Technolojia ya Habari na Mawasiliano na Menejimenti ya Mifumo ya Habari au mafunzo mengine yanayohusiana na fani hii.3.1.2 Kazi za kufanya:-


(a) Kuandaa, kuandika na kufanya majaribio ya program (Plan, Code and test program),


(b) Kusahihisha programu (Debug program),


(c) Kuweka na kuhakikisha usalama wa program (Incorporate security setting into program),


 

(d) Kushirikiana na wadau wengine katika kutengeneza program mbalimbali (corporate with other software developers), na


(e) Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkubwa wake wa kazi zinaendana na sifa na fani yake.3.2 Fani ya Uchambuzi Mifumo ya Kompyuta (Computer Systems Analysis):- (Nafasi 1)


3.2.1 Sifa:-


Waombaji wawe na Stashahada ya Juu au Shahada ya Kompyuta katika moja ya fani zifuatazo; Sayansi ya Kompyuta, na Menejimenti ya Mifumo ya Habari au mafunzo mengine yanayohusiana na fani hii.3.2.2 Kazi za kufanya:-


(a) Kuweka kumbukumbu na taratibu za kisasa na mbinu za kufanyia kazi,


(b) Kutekeleza chati za mtiririko wa mifumo ya nyendo za taarifa na udhibiti,


(c) Kuandika programu za Kompyuta (Implement software systems (write and document code),


(d) Kufanya majaribio ya sehemu timilifu za programu za Kompyuta (Perform unit systems (module testing)


(e) Kufanya majaribio ya usanidi wa mifumo ya TEHAMA (Perform testing of system configurations),


(f) Kufanya majaribio ya program za Kompyuta kulingana na mahitaji ya watumiaji (Conducting user acceptance test), na


 

(g) Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkubwa wake wa kazi zinazaoendana na sifa na fani yake.3.3 Fani ya Usimamizi wa Data za Kielektroniki (Database Administration): - (Nafasi 2)


3.3.1 Sifa:-


Waombaji wawe na Stashahada ya Juu au Shahada ya Kompyuta katika moja ya fani zifuatazo; Sayansi ya Kompyuta, Teknolojia ya Habari, na Technolojia ya Habari na Mawasiliano, Menejimenti ya Mifumo ya Habari au mafunzo mengine yanayohusiana na fani hii.3.3.2 Kazi za kufanya:-

(a) Kutengeneza  kiunganishi  kati ya  hifadhi  data  na


Programu tumizi (Develop back-end and front-end connectivity),


(b) Kusanifu, kutengeneza na kufanya majaribio ya program


za hifadhi-data (Design, implement and test database),


(c) Kuweka usalama wa hifadhi data (Implement security and access control into database),


(d) Kutunza na kuhakiki mfumo wa hifadhi data,


(e) Kutoa huduma za hifadhi data kwa watumiaji,


(f) Kufanya kazi nyingine kadiri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi, na


(g) Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkubwa wake wa kazi zinazoendana na sifa na fani yake.3.4 Fani ya Usimamizi Mitandao ya TEHAMA (Network Administration)-

 


(Nafasi 1)


3.4.1 Sifa:-


Waombaji wawe na Stashahada ya Juu au Shahada ya Kompyuta katika moja ya fani zifuatazo; Uhandisi wa Kompyuta, Sayansi ya Kompyuta Elektroniki na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano au mafunzo mengine yanayohusiana na fani hii.3.4.2 Kazi za kufanya:-


(a) Kusanifu, kusakinisha na kusanidi miundombinu ya ndani na nje ya mtandao wa Kompyuta (Design, install and configure LAN and WAN infrastructure),


(b) Kufanya majaribio ya vifaa vya mtandao wa Kompyuta (Test network equipment and devises),


(c) Kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya usalama wa mtandao kwa mujibu wa miongozo ya usalama wa mtandao wa kompyuta (Implement network security guidelines),


(d) Kutathmini na kurekebisha hitilafu zozote za mtandao wa Kompyuta (Perform network troubleshooting and repair), na


(e) Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkubwa wake wa kazi zinazoendana na sifa na fani yake.


3.5 Fani ya Usimamizi Mifumo ya TEHAMA (System Administration) – (Nafasi 1)


3.5.1 Sifa:-


Waombaji wawe na Stashahada ya Juu au Shahada ya Kompyuta katika moja ya fani zifuatazo; Uhandisi wa Kompyuta, Sayansi ya Kompyuta, Teknolojia ya Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Mifumo ya Habari au mafunzo mengine yanayohusiana na fani hii.3.5.2 Kazi za kufanya:-


(a) Kuchambua na kukusanya mahitaji ya watumiaji wa program ya Kompyuta. (Analyse User Requirements)


(b) Kuandika program za Kompyuta (implement software systems (Write and document code),


(c) Kufanya majaribio ya sehemu timilifu za program za Kompyuta (Perform unit systems (module testing),


(d) Kufanya majaribio ya usanidi wa mifumo ya TEHAMA (Perform testing of system configurations),


(e) Kufanya majaribio ya program za Kompyuta kulingana na mahitaji ya watumiaji (conducting user acceptance test), na


(f) Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkubwa wake wa kazi zinazoendana na sifa fani yake.3.6 Fani ya Usalama wa Mifumo ya TEHAMA (Security Management):- (Nafasi 1)


3.6.1 Sifa:-


Waombaji wawe na Stashahada ya Juu au Shahada ya Kompyuta katika moja ya fani zifuatazo; Uhandisi waKompyuta, Sayansi ya Kompyuta, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Menejimenti ya Mifumo ya Habari au mafunzo mengine yanayohusiana na fani hii.3.6.2 Kazi za kufanya:-


(a) Kusimamia maboresho ya program za kompyuta kwa wakati (Ensure software patches are implemented timely),


(b) Kusakinisha, kusanidi na kuboresha programu za kuzuia virusi vya Kompyuta, (Install, configure and update antivirus software),


(c) Kuelimisha watumiaji masuala mbalimbali yanayohusu usalama, hatari na udhaifu katika mifumo ya TEHAMA (Alert users on various security risks, threats and vulnerabilities),


(d) Kukagua mifumo ya TEHAMA mara kwa mara (Perform systems audit on regular basis),


(e) Kuweka viwango vya usalama na udhibiti katika mifumo ya TEHAMA kwa watumiaji (Implement security mechanism and control in computer systems), na


(f) Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkubwa wake wa kazi zinaendana na sifa na fani yake.Mwisho wa kupokea barua za maombi hayo ni tarehe 1/3/2021 saa 9:30 Alasiri.


Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji zikionyesha anwani sahihi pamoja na namba ya simu na kuambatisha:-


- Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.


- Wasifu wa mwombaji (CV).


- Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.


- Picha mbili za rangi (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni ambazo zimeandikwa majina nyuma yake .


NB. Nakala za vyeti vya taaluma na vya kidato cha nne/sita vithibitishwe na Hakimu/Wakili anayetambuliwa na Serikali (True copies of the originals).


Aidha, inasisitizwa kwamba:-Waombaji wawe na umri kati ya miaka 18 na 44.


Maombi yote yapitishwe kwa Katibu Tawala wa wilaya anayoishi mwombaji.


Waombaji walio katika Utumishi wa Umma wapitishe maombi yao kwa waajiri wao wa sasa.Waombaji walioacha kazi katika Utumishi wa Umma waeleze kwamba waliacha kazi Serikalini na sababu ya kufanya hivyo.


Waombaji watakao shinda usaili na kuajiriwa watakuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wawe tayari kufanya kazi katika mikoa na Wilaya mbalimbali za Tanzania bara.


Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao vithibitishwe na TCU/NACTE.


Waombaji waandike majina yao yote matatu kwa kirefu.


Waombaji waandike nafasi ya kazi wanayoomba nyuma ya bahasha watakazotumia maombi yao.


Waombaji wasiwe walioachishwa/kufukuzwa kazi kwenye Utumishi wa Umma.


     Waombaji ambao wataficha ama kutoonyesha kwenye viambatisho vyao sifa yoyote ya kielimu waliyonayo na ikabainika wakati wa mchakato wa kuwaajiri mchakato huo utasitishwa na hata kama watakuwa tayari wameajiriwa, ajira zao zitasitishwa mara moja.


    Mwombaji asiandike barua zaidi ya moja kwa ajili ya kuomba nafasi moja.


   Waombaji wote wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia mojawapo ya masharti yaliyotajwa hapo juu, maombi yao hayatashughulikiwa.


Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P. 8391,


DAR ES SALAAM.Imetolewa na ;-Katibu,


Tume ya Utumishi wa Mahakama,


S.L.P 8391,


DAR ES SALAAM,