New Post

Friday, February 8, 2019


Image result for tanzania logo
TANGAZO LA
KAZI

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamin
William Mkapa,
inatekeleza Mradi wa Kuimarisha Mifumo Endelevu ya Afya (RSSH)
kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na
Malaria (Global Fund).

Mradi huu una lengo la
kuimarisha huduma za afya ngazi za vituo katika mikoa kumi (10) iliyopewa
kipaumbele na mradi huu ambayo ni; Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Geita,
Kagera, Katavi, Tabora, Dodoma na Kigoma. Kupitia mradi huu, jumla ya wataalamu
281 wamepangwa kuajiriwa kwa kipindi cha mwaka 2018 – 2020 na kupangiwa kufanya
kazi ndani ya mikoa tajwa hapo juu.

Ili kukamilisha ujazaji wa
nafasi za wataalamu zilizobakia wazi, Taasisi ya Mkapa inapenda kutangaza
nafasi wazi 90 za wataalamu wa afya. Nafasi hizi ni kwa ajili ya wataalamu
waliosomea fani za: -

 1. Udaktari nafasi (Nafasi18)
 2. Afisa teknolojia Maabara (Nafasi 4).
 3. Afisa Tabibu (Nafasi 1)
 4. Wateknolojia wasaidizi dawa (Nafasi 34)
 5. Wateknolojia wasaidizi mionzi (Nafasi 21)
 6. Wateknolojia wasaidizi Maabara (Nafasi 2)
 7. Wateknolojia Mionzi (Nafasi 2)
 8. Wauguzi nafasi (Nafasi 7)
 9. Afisa Muuguzi Msaidizi (Nafasi 1)
Sifa za waombaji;

 1. Waliohitimu
  mafunzo kutoka katika vyuo vinavyotambulika na Serikali.
 2. Wataalamu
  wenye vyeti kamili vya mafunzo ya fani walizosomea.
 3. Wataalamu
  wenye leseni hai kutoka katika mamlaka za usajili kwa fani zinazotakiwa
  kufanya usajili kabla ya kuanza kufanya kazi.
 4. Mtanzania
  mwenye umri chini ya Miaka 45.
 5. Wataalamu
  ambao wameajiriwa katika ajira za serikali na za kidini, hawatakiwi kuomba
  ajira hizi.
Maombi yote yaambatanishwe na:

 1. Barua ya maombi ya kazi ikieleza Mikoa
  mitatu ambayo muombaji angependa kupangiwa kufanya kazi katika moja ya
  Halmashauri zake.
 2. Nakala ya cheti cha Taaluma.
 3. Cheti cha kidato cha 4 na 6 kama kipo.
 4. Picha mbilmli (2) – Passport size na
  maelezo binafsi (CV), ikionyesha umri, anuani kamili na namba ya simu ya
  kiganjani, pamoja na anuani/ namba ya kiganjani ya wadhamini wako
  wasiopungua wawili.
 5. Nakala zote za vyeti ziwe zimepitishwa
  na mwanasheria ili kuthibitisha kama ni nakala halisi ya cheti cha
  mwombaji.
Maombi yote yatumwe kwa: Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa, kwa sanduku la Posta 76274 Dar Es Salaam au kwa barua pepe [email protected].
Mwisho wa kupokea maombi ya kazi itakuwa tarehe 28 Februari 2019.

Tangazo hili la kazi
linapatikana pia katika tovuti ya Taasisi ya Mkapa: www.mkapafoundation.or.tz.

 NB: Majibu yatatolewa kwa watakaofanikiwa tu.

IMETOLEWA NA

Afisa Mtendaji Mkuu

Taasisi ya Benjamin
William Mkapa