New Post

Tuesday, July 10, 2018

Orodha ya Majina ya Watumishi wa Afya Waliopangiwa Vituo vya Kazi Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Julai 2018

 

TAMISEMI kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto inapenda kuwataarifu waombaji wa kazi nafasi za afya walioomba kuanzia tarehe 10/05/2018 hadi tarehe 25/05/2018 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilika

Waombaji wote wanatakiwa kuzingatia maelezo yafuatayo

i. Waombaji wote wanatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika muda wa siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo aidha waombaji watakaoshindwa kuripoti katika vituo vya kazi ndani ya siku 14 nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine

ii. Waombaji wote wanatakiwa kuwasilisha vyeti vyao halisi vya kitadto cha nne,sita, chuo NACTE na vyeti vyao halisi vya usajili wa mabaraza ya kitaalamu kwaajili ya kuhakikiwa na mwajiri baada ya kupewa barua ya ajira

iii. Waombaji waliopata nafasi za ajira wanajulishwa kuwa hakutakuwa na nafasi ya kubadlisha vituo vya kkazi walivyopangiwa . watakao shindwa kuripoti katika muda uliopangiwa watakaoshindwa kuripoti katika muda uliopngwa nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine

iv. Waombaji wote ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi hivyo wasisite kuomba tena kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa

v. Waajiri wote mnaelekezwa kuwapokea, kuhakiki na kuwafanyia mafunzo elekezi kabla ya kuwapangaia vituo vya kazi

Orodha ya majina ya waliopangiwa vituo vya kazi inapatikana katika tovuti ya OR-TAMISEMI www.tamisemi.go.tz

pia waweza kubofya hapa