New Post

Wednesday, July 18, 2018

Nafasi za Kazi Halmashauri ya Mji Tunduma,Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 20 July 2018

HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

NAFASI ZA KUJITOLEA ZA MAAFISA UANDIKISHAJI WA MFUKO WA AFYA YA JAMII CHF (NAFASI 71)

Mkurugenzi wa Mji Tunduma anawatangazia wananchi wote kuwa Halmashauri ya Mji Tunduma, katika kutekeleza Waraka Namba 1 wa Maboresho ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), kutakuwa na
nafasi za kujitolea za Maafisa Uandikishaji (Enrollment Officers).
Kila Afisa Mwandikishaji mmoja atapangwa katika mtaa anaoishi ndani ya Mji wa Tunduma na
atafanya kazi ya kusajili kaya katika mfuko wa CHF katika mtaa wake. SIFA ZA MWOMBAJI

1. Awe ni raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 21 au zaidi
2. Awe ni mkazi wa Tunduma, kata na mtaa husika
3. Awe na sifa za kuaminika na kuaminika miongoni mwa jamii anayoishi
4. Awe amepitia zoezi la ePRS. Endapo katika Mtaa husika hakuna mwandikishaji wa zoezi la
ePRS ateuliwe mwandikishaji mwingine
5. Awe anamiliki simu janja (smartphone)
6. Asiwe mwajiriwa wa taasisi yo yote
7. Awe amehitimu elimu ya kidato cha nne, sita na kuendelea
8. Awe na moyo wa kujituma na kujitolea, na anayejihusisha na masuala ya maendeleo katika
mtaa husika
Ajira hizi ni za mkataba wa miezi kumi na mbili, na mkataba unaweza kuhuishwa mara baada ya
kipindi hicho kuisha, kadiri mamlaka husika itakavyoona inafaa. Mwandikishaji huyu hatalipwa
mshahara, bali kamisheni kutokana na idadi ya kaya alizoandikisha kwa mujibu wa mwongozo uliopo.

JINSI YA KUOMBA
1. Barua ya maombi
2. Wasifu (CV)
3. Nakala ya vyeti vya taaluma
4. Nakala ya vyeti vya ujuzi mwingine kama vipo
5. Picha mbili za rangi za hivi karibuni
Barua zote za maombi ziwasilishwe kwa mkono katika Masijala ya Halmashauri ya Mji Tunduma kwa
Anwani ifuatavyo:

Mkurugenzi wa Mji
Halmashauri ya Mji Tunduma
S.L.P. 73
2
TUNDUMA

Mwisho wa kupokea maombi ni siku ya Ijumaa, tarehe 20 Julai 2018, saa 9:30 mchana.
Aidha, tangazo hili linafuta tangazo lililotolewa tarehe 13 Julai 2018. Tafadhali kabla ya kutuma
maombi zingatia maelekezo.

Imetolewa na
Ndugu Kastori G. Msigala
KAIMU MKURUGENZI WA MJI
HALMASHAURI YA MJI TUNDUMA

NB: tangazo hili pia linapatikana katika mtandao wa www.tundumatc.go.tz