New Post

Friday, July 20, 2018

Nafasi za Kazi Halmashauri ya Jiji la Arusha, Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 9 Agusti 2018

Halmashauri ya Jiji la Arusha

Kumb Na. CD/E.30/2VOL.III/89

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI

Halmashauri ya Jiji la Arusha imepokea kibali cha Ajira mpya chemye kumbukumbu namba FA. 170/371/01/III cha tarehe 22/06/2018 kwa mantiki hiyo Mkurugenzi wa Jiji anawatangazia nafasi za kazi Watanzania wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Jiji la Arusha kutuma maombi ya kazi kwa Mkurugenzi wa jiji ndani ya siku 21 kuanzia tarehe ya tangazo

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II (NAFASI 1)

SIFA/ELIMU/UJUZI
- Awe Raia wa Tanzania na mwenye akili timamu
- Awe na elimu ya kidato cha IV/VI
- Awe na umri usiopungua miaka 18 na usizidi miaka 45
- mwenye cheti cha utunzaji kumbukumbu katika mojawapo ya fani za Afya, Masijala, na Mahakama ya Ardhi

KAZI NA MAJUKUMU
• Kutafuta kumbukumbu/ nyaraka/ majalada yanayohitajiwa na wasomaji
• Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/ nyaraka
• Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/ nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi
• Kuweka/kupanga kumbukumbu/ nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhiwa kumbukumbu
• Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka, na kaadharika) katika majalada
• Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/ nyaraka kutoka Taasisi za Serikali

NGAZI YA MSHAHARA TGS B SAWA NA 390,000/= kwa mwez

==========================

KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III – NAFASI 1

SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe Raia wa Tanzania na mwenye akili timamu
- Awe na elimu ya kidato cha IV/VI
- Awe na umri usiopungua miaka 18 na usizidi miaka 45
- AWE amefahulu somo la hati mkato ya kiswahili na kingereza maneno 80 kwa dakika moja
- Awe amepata mafunzo ya kompyuta kutoka katika chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti chenye programu za WINDOWS, MS OFFICE, INTERNET, EMAIL na Pulbisher

MAJUKUMU YA KAZI

• Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
• Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
• Kusaidia kutunza taarifa / kumbukumbu zamatukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba na kazi zingine. Zilizo pangwa kutekelezwa katika ofisi anamo fanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwawakati unao hitajika.
• Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinacho hitajika katikashughulizakazihapoofisini.
• Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
• Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazo husika.
• Kutekeleza kazi zozote atakazo kuwa amepangiwa na Msimamizi wake wakazi.

NGAZI YA MSHAHARA TGS B SAWA NA 390,000/= kwa mwez

=======================

DRERVA DARAJA LA II NAFASI 4

SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe Raia wa Tanzania na mwenye akili timamu
- Awe na elimu ya kidato cha IV/VI
- Awe na umri usiopungua miaka 18 na usizidi miaka 45
- Awe na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja
- Awe na Leseni dalaja la C na E ya uendeshaji magari
- Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji wa magari Basic Driving Course yanayotolewa na chuo cha usfndi stadi VETA au chuo kingine kinachotambulika na Serikal
- Mwombaji mwenye cheti cha majaribio ya ufundi darafa la II watafikiriwa

MAJUKUMU
- kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari
- kuwapeleka watumishi maeneo mbali mbali kwenye safari za kikazi
- Kufanya matengenezo madogomadogo katika gari.
- kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
- Kutunza na kuandika daftari la safari
- kufanya usafi wa gari na
- kunfanya kazi nyingine atakayopangiwa na msimamizi wake

NGAZI YA MSHAHARA TGS B SAWA NA 390,000/= kwa mwez

MAELEZO YA JUMLA
- Barua ya maombi iambatanishwe na CV yenye wadhamini watatu wenye anuani na namba za simu, nkala za vyeti vya elimu, nakala za vyeti vya kuzaliwa, picha 2 na baurua ziandikwe namba ya simu ya muombaji andika nafasi unayoomba nyuma ya bahasha
- mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 09/08/2018
- maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo

Mkurugenzi wa Jiji,
Halmashauri ya Jiji la Arusha,
S.L.P 3013
ARUSHA