New Post

Tuesday, July 31, 2018

Nafasi Mbali Mbali za Kazi Utumishi, Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 13 Agosti, 2018

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/ I/164 30 Julai, 2018

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Shirika la Mzinga anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza
nafasi wazi za kazi 23 kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.

1.0 MWENYEKITI WA MABARAZA YA ARDHI NA NYUMBA LA WILAYA
(CHAIRPERSON) – NAFASI 20

1.1 MAJUKUMU
i. Kusikiliza kuamua migogoro yote ya Ardhi na Nyumba kwa Mujibu wa Sheria Na.2 ya Mwaka 2002;
ii. Kusikiliza na kutoa uamuzi Rufaa kutoka Mabaraza ya Kata;
iii. Kufanya marejeo kwa mashauri yaliyosikilizwa na Mabaraza ya Kata; na
iv. Kusimamia utekelezaji wa Maamuzi ya Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya na Mabaraza ya Kata yaliyo kwenye eneo husika.

1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
i. Awe na Shahada ya Sheria na kuendelea kutoka Chuo Kikuu
kinachotambuliwa na Serikali na kumaliza mafunzo kazini (Internship) au
Postgraduate diploma kutoka Shule ya Sheria Tanzania;
ii. Awe mwaminifu, awe na msimamo na mtu asiyeweza kuyumbishwa;
iii. Awe hajawahi kushitakiwa katika Mahakama yeyote na kupatikana na hatia; na
iv. Awe na uzoefu wa miaka mitano (5) katika masuala ya Sheria na kutolea
uamuzi

1.3 Mashahara: LSSE. 2

2.0 FUNDI MCHUNDO DARAJA II (USUBIAJI NA UUNGAJI VYUMA-MOULDING) -
NAFASI 2 (LINARUDIWA)

2.1 MAJUKUMU YA FUNDI MCHUNDO DARAJA II (USUBIAJI NA UUNGAJI
VYUMA-MOULDING)
i. Kuandaa mchanga utumikao katika uandaaji wa „moulds‟ na „core‟ mbalimbali;
ii. Kutengeneza „moulds‟ za aina mbalimbali kwa ajili ya usubiaji;
iii. Kusubu brasi na vyuma;
iv. Kushirikiana na wafanyakazi wengine katika kutimiza malengo ya Shirika; na
v. Kufanya kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Kiongozi wake.

2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Elimu ya kidato cha nne na Cheti cha Ufundi Stadi (Trade Test Grade III/CBET I)
yenye mwelekeo wa Usubiaji na Uungaji Vyuma „moulding‟ kutoka VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Mashirika ya Umma PGSS

3.0 FUNDI MCHUNDO DARAJA II (UUNDAJI WA PATENI) -NAFASI 1 (INARUDIWA)

MAJUKUMU
i. Kusoma na kutafsiri michoro;
ii. Kutambua tabia mbalimbali za mbao zinazotumika kutengenezea pateni;
iii. Kutengeneza pateni na „core boxes;
iv. Kukarabati pateni na „core boxes‟;
v. Kushirikiana na wafanyakazi wengine katika kutimiza malengo ya Shirika; na
vi. Kufanya kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Kiongozi wake.

3.1 SIFA ZA MWOMBAJI
Elimu ya Kidato cha Nne na Cheti cha Ufundi Stadi (Trade Test Grade III/CBET I) yenye
mwelekeo wa Uundaji wa Pateni “Pattern Maker” kutoka VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

3.2 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Mashirika ya Umma PGSS 2.

MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45;
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa;
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo;
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika;
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA;
vi. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa
na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU au NECTA);
vii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi
kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi;
viii. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010;
ix. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria;
x. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 13 Agosti, 2018;
xi. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.
xii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia
inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

MUHIMU: KUMBUKA KUAMBATISHA BARUA YAKO YA MAOMBI YA KAZI
ILIYOSAINIWA PAMOJA NA VYETI VYA ELIMU. ANUANI YA BARUA HIYO
IELEKEZWE KWA:
KATIBU, OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
S.L.P 63100
DAR ES SALAAM.
LIMETOLEWA NA
KATIBU SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA