New Post

Tuesday, July 17, 2018

AJIRA MPYA ZA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI, JULAI, 2018

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WA
SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI JULAI, 2018

Ofisi ya Rais - TAMISEMI inapenda kuutarifu Umma kuwa, jumla ya
Walimu 4,840 wamepangiwa vituo vya kazi kwenye Shule mbalimbali
za Msingi na baadhi kwenye Shule za Sekondari nchini. Walimu hao
waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuripoti katika Ofisi za
Wakurugenzi wa Halmashauri zilipo shule walizopangiwa na baadaye
kuripoti kwenye Shule walizopangiwa. Walimu wote wanatakiwa
kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi kuanzia tarehe 23 Julai, 2018
hadi tarehe 7 Agosti, 2018 wakiwa na mahitaji yafuatayo:

(i) Vyeti halisi vya taaluma vya Kidato cha Nne na/au Kidato cha
Sita;

(ii) Vyeti halisi vya kitaaluma vya mafunzo ya Ualimu katika ngazi
husika; na
(iii) Cheti halisi cha kuzaliwa.
Walimu wote waliopangiwa vituo vya kazi wanaelekezwa kuwa:

i. Vituo vyao vya kazi ni Shule ya Msingi au Sekondari
alizopangiwa na sio Makao Makuu ya Halmashauri;

ii. Mwajiriwa atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu kisha
akaondoka katika kituo chake cha kazi alichopangiwa Serikali
itamchukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria na taratibu
zilizopo; na

iii. Hakuna Mwalimu atakayekubaliwa kubadilisha kituo kwa
sababu yoyote ile. Kila mwajiriwa mpya anapaswa kuripoti
katika kituo chake alichopangiwa na si vinginevyo. Waajiriwa
wapya ambao watashindwa kuripoti katika vituo
walivyopangiwa nafasi zao zitachukuliwa na Walimu wengine
5,220 wenye sifa waliokosa nafasi.

Wakurugenzi wa Halmashauri husika wawapokee Walimu
waliopangwa kwenye Halmashauri zao kwa kuzingatia taratibu na
kanuni zote za utumishi wa Umma, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa
ya kuripoti kwao. Taarifa ya kuripoti waajiriwa hao itumwe Ofisi ya
Rais- TAMISEMI ifikapo au kabla ya tarehe 10.08.2018 baada ya tarehe
ya mwisho ya kuripoti.

Majina ya Walimu waliopangiwa vituo yanapatikana katika tovuti ya
Ofisi ya Rais - TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
Imetolewa na:
KATIBU MKUU
OFISI YA RAIS - TAMISEMI

bofya hapa kuweza kuona majina hayo