New Post

Friday, June 1, 2018

Tangazo la Nafasi za Kazi Kada ya Afya Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 4 Juni 2018

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za Kazi katika kada za afya kama ifuatavyo

TABIBU WA MENO II NAFASI 1

SIFA ZA MUOMBAJI
- Kuajiriwa awe mwenye elimu ya kidato cha 4 au 6 aliyehitimu mafunzo ya stashahada ya udaktari katika chuo cha Serikali na chuo chochote kinachotambulika na Serikali

MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali TGHS B

TABIBU DARAJA LA II NAFASI 1

SIFA ZA MWOMBAJI

- Kuajiriwa mwenye elimu ya kidato cha 4 au 6 na aliyehitimu mafunzo ya shtashahada ya udaktari wa binadamu katika chuo cha Serikali au chochote kinachotambuliwa na Serikali

MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali TGHS B

TABIBU MSAIDIZI NAFASI 10

SIFA ZA MWOMBAJI

- Kuajiriwa mwenye elimu ya kidato cha 4 au 6 na aliyehitimu mafunzo ya shtashahada ya Mionzi wa binadamu katika chuo cha Serikali au chochote kinachotambuliwa na Serikali

MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali TGHS B

MUUGUZI DARAJA LA II NAFASI 10

SIFA ZA MWOMBAJI
- Kuajiriwa mwenye elimu ya kidato cha 4 au 6 na aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/cheti ya uuguzi na ukunga katika chuo cha Serikali au chochote kinachotambuliwa na Serikali

MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali TGHS A

MTEKNOLOJIA RADIOLOJIA NAFASI 1

SIFA ZA MWOMBAJI

- Kuajiriwa mwenye elimu ya kidato cha 4 au 6 aliyehitimu mafunzo ya stashahada ya mionzi katika chuo cha Serikali na au chuo kinachotambulika na Serikali

MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali TGHS B

KATIBU WA AFYA DARAJA LA II NAFASI 1

SIFA ZA MWOMBAJI
- Mwenye elimu ya kidato cha 4 au 6 na aliyehitimu mafunzo ya shahada ya kwanza ya Menejimenti ya Afya katika chuo cha Serikali na vyuo vinavyotambulika na Serikali

MUHUDUMU WA AFYA NAFASI 1

SIFA ZA MWOMBAJI
- Mwenye elimu ya kidato cha 4 aliyehitimu mafunzo ya astashahada au cheti katika fani ya utunzaji kumbu kumbu za afya katika chuo cha Serikali au chuo chochote kinachotambulika na Serikal atapewa kipaumbele

MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali TGHOS A

MASHARTI YA JUMLA

i/ Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 20 hadi 45
ii/ Waombaji waambatanishe vyeti vya kuzaliwa
iii/ Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika kada tofauti na walizonazo barua za maombi yao yapitishwe kwa waajiri wao
iv/ Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza yenye anuani zao, namba za simu za kuaminika na majina ya wadhamini watatu wa kuaaminika
v/ Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma na vyeti vya kidato cha 4 au 6 kwa wale waliofika huko na wenye kuhitimu mafunzo mbali mbali kwa kuzingatia kazi husika pia iambatanishwe paspoti ya hivi karibuni na iandikwe majina matatu kwa nyuma
vi/ Testimonials, provisional results, statement of results, na hati za matokeo ya kidato cha 4 na 6 hazitakubaliwa
vii/ wAOMBAJI WALISTAAFISHWA KATIKA UTUMISHI WA UMMA hawataruhusiwa kuomba isipokuwa kwa kibali cha katibu Mkuu Kingozi
viii/ Uwasilishwaji wa sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria
ix/ Maombi yaandikwe kwa mkono wa mwombaji na kwa lugha y Kiswahili au Kingereza
x/ Waombaji wote kwenye barua zao za maombi waandike namba za simu za uhakika kwaajili ya mawasiliano

maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo

MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA,
S.L.P 73,
CHUNYA.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 04/06/2018