New Post

Friday, June 22, 2018

Nafasi za Kazi Muuguzi II - Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 25 Juni 2018

Halmashauri ya Wilaya ya Pangani

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani anapenda kuwatangazia wananchi wote watanzanai wenye sifa za kujaza nafasi za kazi kwa kada ya afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani

Muuguzi II (Nafasi - 6)

Sifa za Mwombaji
- Awe amahitimu elimu ya kidato cha 4 au 6
- awe amehitimu mafunzo ya uuguzi katika chuo kinachotambuliwa na Baraza la wauguzi na Wakunga Tanzania au mafunzo ya uuguzi katika ngazi ya cheti na wenye uzoefu wa kazi wa muda usiopungua miaka miwili

Kazi na Majukumu
i/ Kufanya kazi za kiuuguzi za kuhudumia wateja katika jamii hospital na sehemu zote zinapotolewa huduma za afya
ii/ Kukusanya takwimu na kutayarisha taarifa za utendaji kazi
iii/ Kufuatilia matatizo ya kiafya ya wagonjwa na jamii katika mazingira yao
iv/ Kutoa huduma za chanjo kwa mama wmtoto na uzazi alama
v/ kusimamia, kuratibu na kufuatailia kazi za waliochini yake
vi/ Kufuatilia utunzaji wa vifaa na vitendea kazi katika maeneo yake ya kazi
vi/ kufanya kazi zingine atakazo pangiwa na mkuu wake wa kazi

Mshahara kwa mwezi Tshs 680,000/=

aidha mwombaji wa nafasi hizo anatakiwa kuzingatia yafyatayo

- Mwombaji ambaye hana sifa anashauriwa kutoomba sababu barua yake haitshughulikiwa
- mwombaji aandike barua yake ya maombi mwenyewe kwa mkono na ambatanishe wasifu, vivuli vya vyeti vyake vya taaluma na cheti cha kuzaliwa na picha mbili za passport size
- mwombaji awe tayari kufanya kazi katika mazingira ya vijijini
- mwombaji anatakiwa awe na umri usiozidi miaka 45
- barua zote ziadikwe kwa Mkurugenzi na zitumw kabla ya tarehe 25/06/2018

barua zitumwe kwa anuani ifuatayo

Mkurugenzi Mtendaji,
S.L.P 89,
PANGANI