New Post

Saturday, June 30, 2018

Nafasi za Kazi Meneja, Karani wa Mahesabu & Muhudumu - Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (Meatu), Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 10 Agosti 2018

Halmashauri ya Wilaya ya Meatu

Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Kinyaki Teachers Saccos Limited SHR.1019

Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Kinyaki Teachers Saccos Limited kinakaribisha maombi ya Kazi kwa nafasi zifuatazo

MENEJA NAFASI 1

SIFA ZA MWOMBAJI
i/ mwanamke/au mwanaume raia wa Tanzania
ii/ Elimu awe na geree ya uhasibu na utawala
iii/ Umri kuanzia miaka 22 mpaka 45
iv/ Awe na uwezo wa kutumia kompyuta ni sifa muhimu

MSHAHARA
Mshahara wa kuanzia utakuwa ni makubalino kati ya mwajiri na mwajiriwa

MAJUKUMU

- kuandaa na kutunza vitabu vya mahesabu na kumbukumbu nyingine muhimu za chamani
- kupokea fedha yote inayolipwa chamani na kufanya malinganisho ya fedha iliyopokelewa na iliyolipwa kila siku
- kufanya malipo yote baada ya kupata kibali cha bodi
- kukusanya marejesho ya mikopo na faida ya chama
- kufanya malinganisho ya hesbu ya benki kila mwaka
- kuandaa taarifa ya kila mwezi ya hali ya fedha na takwimu zote
- kuwapigia hesabu ya mkopo wanachama wanaokopa
- kufuata masharti na kanuni za fedha na uandishi wa vitabu
- kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na bodi

KARANI MAHESABU (ACCOUNTS CLERK) NAFASI 1

SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe raia wa Tanzania
- Awe na elimu ya Diploma ya uhasibu na kujiendeleza katika fani za biashara kama vile utunzaji wa hesabu (ATC I na ACTEC II)
- Umri kati ya miaka 22 na 45
- Awe na uwezo wa kutumia kumpyuta

MSHAHARA

Mshahara wa kuanzia ni makubaliano kati ya mwajiri na mwajiriwa

MAJUKUKU
a) Kupokea na kutunza katika mali ya usalama fedha zote zinazoingia chamani
b) kuandika vitabu vya mahesabu
c) kuamdaa taarifa za mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima zinazohsu fedha
d) kuandaa urari na mizani ya chama kila mwezi
e) Kufanya malipo yote ya fedha kwa kuzingatia idhini iliyotolewa na bodi/ meneja
f) Kuwasaidia wananchama kujaza fomu za maombi ya uanachama na maombi ya mkopo
g) Kufanya kazi nyingine kama atakavyopangiwa na bodi

MUHUDUMU WA OFISI NAFASI 1

SIFA ZA MUOMBAJI
- Awe mwanamke au mwanaume raia wa Tanzania
- Awe na umri usiopungua miaka 22-35
- Awe amemaliza kidato cha 4 au zaidi
- Awe anafahamu kumpyuta

MAJUKUMU

1 Kuchapa nyaraka za ofisi
2. Kufanya usafi ofisini
3. Kutunza mali za chama na nyaraka za ofosini wakati wote wa kazi
4. na majukumu mengine atakayopewa na karani, meneja au mwajiri wake

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
- Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji mwenyewe (zisichpwe)
- mambo yaambatanishwe na vivuli vya vyeti vya elimu ya sekondari na vyuo kwa waliopitia vyuoni pamoja na taarifa nyingine binfsi
- muombaji ataje majina mawili ya watau wanaomfahamu vizuri (referees) anwani na namba zao za simu
- picha 2 za passport size za hivi karibuni
- ambatanisha namba yako ya simu ya mkononi au ya mtu wako wa karibu katika mawasiliano yako, FAX au anuani ya barua pepe , mawasiliano hayo ni muhimu katika kuwaita wahusika kenye usaili

barua za maombi zitumwe kwa anuani ifuatayo

MWENYEKITI NA WAJUMBE WA BODI,
KINYAKI TEAHERS SACCOS LIMITED,
S.L.P 296,
MWAHUNZI - MEATU

Barua pia zinaweza kuwasilishwa moja kwa moja ofisi ya KINYAKI SACCOS LTD, MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 10/08/2018 SAA 10 JION