New Post

Friday, June 8, 2018

Nafasi za Kazi Account Assistant - Mkoa wa Mwanza Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 18 June 2018

OFISI YA MKUU WA MKOA WA MWANZA

Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza anawatangazia nafasi za kazi ya mkataba kada ya Mhasibu Msaidizi (Nafasi 9). Hivyo waombaji wenye sifa wanatakiwa kutuma maombi ya nafasi hiyo ya kazi

Mhasibu Msaidizi Nafasi 9

Ngazi ya Mshahara ni TGS B1

Sifa za Kujiriwa
- Wenye eleimu ya kidato cha 4 aliye hitimu mafunzo ya uhasibu katika nagazi ya cheeti katika chuo kinachotambuliwa na serikali
- Uzoefu wa Kutumia Kompyuta

Kazi/Majikumu ya Kufanya

i/ Kukusanya mapato kwa njia ya kieletroniki / kadi za wateja wanaofika hospitali kupima afya
ii/ Kuwasilisha taarifa za maukusanyo ya kila siku kwa Casahier hospital
iii/ kutoa taarifa haraka iwezekanavyo kwa msimamizi inapotokea changamoto ya mfumo

Mambo ya Kuzingatia kwa Waombaji
- Awe raia wa Tanzania kuanzia miaka 18 mpaka 45
- waombaji lazima waambatanishe nakala za vyeti vifuatavyo
a). cheti cha taaluma ya uhasibu ngazi ya cheti
b). cheti cha kidato cha 4
c). cheti cha mafunzo ya matumizi ya kompyuta
d). cheti cha kuzaliwa
e). picha 2 passport size za hivi karibuni
f). RESULT SLIP AU PROVISIONAL HAVITAKUBALIWA
g). waombaji wenye vyeti vya kidato cha 4 au vya taaluma kutoka nje wahakiishe vimehakikiwa na NECTA na NACTE
H). Waombaji ambao ni watumishi wa Umma hauruhusiwi kuomba nafasi hizi
i). kuwasilisha vyeti vya kughushi na maelezo mengine itasababisha kuchukuliwa hatua za isheria
j). Barua za maombi ziandikwe kwa Kiswahili au Kingereza
k). WATAKAO CHAGULIWA KUFANYA USAILI WATAJULISHWA TAREHE YA USAILI
l). tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni tarehe 18 Juni 2018 saa 9 Alasiri
- Waombaji wanatakiwa kuwasilisha wasifu binafsi ukionysha mawasiliano ya wahusika, namba za simu na wadhamini watatu

maombi yatumwe kwa njia ya barua kutumia nuani ifuatayo

KATIBU TAWALA,
S.L.P 119,
MWANZA