New Post

Saturday, June 2, 2018

Nafasi ya Kazi Sales Representatives (Afisa Mauzo) - Platinum Credit Ltd, Tuma Maombi Yako Mapema

Sales Representatives (Afisa Mauzo)

Job Description

Platinum Credit Ltd ni kampuni inayotoa huduma ya mikopo ya dharura kwa watumishi wa serikali ya Tanzania na Taasisi zilizo thibitishwa.Kampuni imejizatiti kuhakikisha huduma zake kwa wateja zinapatikana ndani ya muda wa saa 24.

Katika kuimarisha juhudi zake za kutoa huduma inayoridhisha kwa wateja wake, Kampuni inatangaza fursa ya ajira kwa vijana watanzania kama ifuatavyo:

i. Nafasi : Afisa Mauzo ( Nafasi 60)

ii. Eneo la kazi: DAR ES SALAAM

iii. Majukumu
a) Kupanga sehemu ya kwenda kufanya mauzo
b) Kushiriki katika shughuli za masoko na kutangaza bidhaa za kampuni
c) Kujibu maswali ya wateja
d) Kusaidia wateja kujaza fomu pamoja na nyaraka zinazo hitajika
g) Kufuatilia wateja waliohama /wasio lipa
h) Kushirikiana na viongozi wa tawi kuidhinisha na kuingiza makato kwa mwajiri kwa kila mkopo

iv. Sifa za muombaji
a) Awe na elimu isiyo chini ya kidato cha Nne.
b) Awe mwenye kujituma kutafuta masoko na kuhudumia wateja
c) Awe na utayari na uwezo wa kujifunza kazi kwa haraka.
d) Awe na uwezo wa kuongea vizuri Kiswahili
e) Awe na lugha nzuri ya kuongea na wateja na kushirikiana na wafanyakazi wenzake.
f) Awe mwaminifu kwa wateja na kujitambua katika kazi na maisha binafsi.
g) Awe na umri usiopungua miaka 20.

v. Jinsi ya kutuma maombi
Muombaji anaweza kutuma maombi yake kwa njia mojawapo ya hizi zifuatazo:
a) Barua pepe(Email): [email protected] [email protected]
b) Namba ya simu: 0652-746330 / 0716-100699 / 0677-700586

a)*Maombi yaambatane na:
 Nakala ya wasifu wa muombaji(CV)
 Nakala ya veti vya muombaji,
 Picha ndogo(passport size) mbili za karibuni.

TO APPLY ONLINE CLICK HERE