New Post

Friday, June 8, 2018

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Utumishi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/I/143 07 JUNI 2018

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya
Vocational Educational and Training Authority (VETA), Ministry of Lands,
Housing and Human Settlements Development, Tanzania Cotton Board,
Development Of Educational Management (ADEM), Carmatec, Wizara na
Mamlaka za Serikali za Mitaa anapenda kuwataarifu waombaji kazi katika
Taasisi zilizotajwa kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe
12-19Juni, 2018 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi
watakaofaulu usaili.

Waombaji kazi wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia
maelekezo yafuatayo:-

i. Usaili wa Mchujo unatarajiiwa kufanyika tarehe 12 Juni,
2018 kama ilivyoainishwa kwenye ratiba ya usaili kwenye
tangazo hili.

ii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.

iii. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na: Kitambulisho cha
Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi,
Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.

iv. Wasailiwa wanatakiwa kufika na Vyeti Halisi vya kuanzia kidato
cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu,
Shahada ikiwa na “Transcript” yake na kuendelea
kutegemeana na sifa za Mwombaji.

v. Wasailiwa watakaokosa Vyeti halisi na badala yake kuwasilisha
“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati
matokeo za kidato cha IV na VI (FORM IV AND FORM VI
RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA
KUENDELEA NA USAILI.

vi. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.

vii. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanya
usaili.
viii. Kila Msailiwa afike na picha yake „passport size‟

ix. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzaniawahakikishe Vyeti
vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU
na NECTA)

x. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo
hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo wasisite kuomba
tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa.

Kusoma majina hayo tembelea tovuti ya ajira.go.tz